Beyonce na lile kundi lake la destiny child wahamia kwenye gospel.. cheki video hapa..

SOCIALIZE IT ⇨
 bey

Kundi la destiny child liliundwa na Beyonce Knowles, Kelly Rowland pamoja Michelle Wiliums na kuamua kusambaratika huku kila mmoja akijitegemea na kuendelea na kazi zake za muziki.

Mara ya mwisho kundi hili lilishirikiana mwaka 2013 lakini unaambiwa mwishoni mwa juma hili waliungana tena katika tuzo za 30 za kila mwaka za muziki wa injili za Stellar zilizofanyika katika ukumbi wa Las Vegas Orleans Arena.
destiney

Wadada wo walipanda jukwaani na kuimba pamoja wimbo wa “When Jesus Say Yes”ambao ni wa Michelle aliowashirikisha wenzake.

Wimbo huo ulishinda vipengele vitatu ambavyo ni wimbo bora wa mwaka,video bora huku Michelle akishinda tuzo ya mwanamke mwenye sauti katika albam yake ya ‘Journey to freedom’.
stellar

Tuzo ya wimbo wa Say Yes alishinda Michelle akimshirikisha Beyonce pamoja na Kelly na si kama kundi la Destiny child na walikuta wakikutana wote ambao walitoka kundi moja kitendo ambacho hakikupangwa.

Video ya nyimbo hiyo inatarajia kutoka rasmi April 5 siku ya pasaka.

0 comments:

Post a Comment