Huwa unadata na nyumba nzuri nzuri? cheki hizi hapa ni balaaa..

SOCIALIZE IT ⇨


a2
Furaha nyingine kubwa kwa watu mbalimbali nikiwemo mimi ni kuishi au kukaa kwenye sehemu ambayo moyo wangu umeridhia, yani kuanzia mazingira yanayozunguka hapo ndio maana kwenye ndoto zangu za ujenzi siwezi kuacha kupitapita nione idea ipi itanivutia.

Ujenzi wa nyumba nzima kama hizi unaweza kuwa kikwazo kwako sababu ya kipato lakini mimi na wewe tunaweza kupata idea hata chache za kuhamishia kwenye nyumba za uwezo wetu na bado tukawa washindi.
a1
Kwenye hii nyumba ya kwanza nimevutiwa na jinsi walivyoweza kucheza na ukuta mweupe kwa kuweka vitu ukutani na ndio ukavutia zaidi.
a3
Wakati mwingine sebule sio lazima iwe na vitu viiiiingi ndio ivutie, kama hii nimeipenda sana
a4
a5
a6
a7
Siku hizi bongo naona watu wengi wanakwepa rangi nyeupe na kuweka blue au kijani, labda huyu mwenye hii nyumba ameweza kubadilisha mtazamo wetu
Hii nyumba ya pili ni kwa wale watu wangu wanaopenda kuwa na nafasi kubwa nyumbani.
a8
a9
a10
a11
Hii sebule imenivutia jinsi walivyo tumia ubunifu kuweka kochi moja badala ya kuweka matatu ambapo pasingetosha.
a12
a13
a14
a15
a16
a17
a18
Hakuna haja ya kuwa na kabati la TV ndio uonekane wa kisasa, uwekaji wa TV kwenye ukuta ndio wa kisasa zaidi au kuwa na kabati dogo kama hili.

a19
a20
a21
a22
a23
a24
a25
a26

Chumbani hakuna meza ya kufanyia kazi wala kochi la kupumzika, uhuru ni wako na kitanda.

0 comments:

Post a Comment