Jinsi ya kuzuia Mimba kwa Njia ya Kalenda, Jifunze Hapa.
JINSI YA KUZUIA MIMBA KWA KUTUMIA KALENDA
KUNA wasomaji walioniomba niandike juu ya jinsi ya kuitumia kalenda katika kuzuia mimba. Nimeona nifanye hivyo leo lakini kabla sijaenda kwenye kuizungumzia njia hiyo, nieleze kwa ufupi athari za kutumia vidonge vya kuzuia mimba.
Mwanamke anapotumia vidonge hivyo kwa mara ya kwanza anaweza kukumbwa na hali ya machafuko tumboni, kutapika wakati wa asubuhi, kuvimba matiti kama siyo kukumbwa na dalili za ujauzito.
Sambamba na hilo, watumiaji wengine wa vidonge hutokwa na damu nyingi wakati wakiwa kwenye siku zao.
Athari kubwa anayoweza kuipata mtumiaji wa vidonge vya kuzuia mimba ni kuganda kwa damu kwenye moyo, mapafu au ubongo.
Hizo ni athari za kutumia vidonge vya kuzuia mimba hivyo unatakiwa kuwa makini sana ili kutojitafutia matatizo yanayoweza kuepukika.
Baada ya kugusia kidogo hilo, sasa nirejee kwenye namna mwanamke anavyoweza kutumia kalenda katika kuzuia mimba.
Njia hii si ya uhakika sana lakini ni nzuri kwa sababu haina gharama. Njia hii huwafaa zaidi wanawake ambao taratibu za siku zao za kwenda mwezini ni kawaida, yaani mara moja kila baada ya siku 28.
Ili iweze kuzaa matunda, njii hii huhitaji mtumiaji awe tayari kukaa bila kukutana kimwili kwa muda wa wiki moja kila mwezi!
Kwa kawaida kuna siku 8 tu kila mwezi ambazo mwanamke anaweza kupata mimba ambapo siku hizi zipo katikati ya siku zake za kwenda mwezini na huanza siku 10 baada ya siku ya kwanza ya kupata damu ya hedhi.
Hivyo ikiwa mwanamke hataki kupata mimba ni lazima aache kukutana na mwanaume kwenye siku hizi 8! Naamini hili linawezekana kwani siku nyingine zilizobakia wapendanao wanaweza kujiachia kama kawaida.
Ili kuepukana na ‘kuchanganya madawa’, ni lazima mwanamke aonyeshe kwenye kalenda zile siku ambazo hatakiwi kukutana na mwanaume.
Kwa mfano: Unaingia kwenye siku zako tarehe 5 Desemba, weka alama kwenye tarehe hiyo kisha hesabu siku 10 na baada ya hapo pigia msitari siku 8 zinazofuata!
Kumbuka siku hizo nane utakazozipigia msitari ni hatari kwani ukikutana na kidume cha ‘mbegu’ tu na kushiriki ngono bila kutumia kondom utashika mimba, hivyo ni vema usikutane na mwanaume hata kidogo.
Yaani epuka kabisa kufanya ngono bila kondom katika kipindi hicho na hata mpenzi wako akikulainisha kwa lugha ya kimahaba kwa kukuambia kuwa ‘atapiz’ nje.
Kumbuka suala la ‘kupiz’ nje (withdraw method) ni ngumu sana kwa wanaume walio wengi licha ya kwamba ikitumika kiufasaha pia inaweza kusaidia.
Nimalize kwa kusema kuwa, mwanamke anapaswa kuendelea na utaratibu huu kila mwezi lakini akumbuke kuwa, njia hii haina uhakika sana mpaka itumiwe sambamba na njia nyingine kama vile kondom.
0 comments:
Post a Comment